Wimbo wa Maria.- MAGNIFICAT 😇
Luka 1:46-55
46 Naye Maria akasema:
Nafsi yangu inamtukuza Bwana,
47 Na roho yangu inafurahi katika Mungu Mwokozi wangu,
48 Kwa kuwa ameyatazama unyonge wa mjakazi wake;
Maana tazama, toka sasa vizazi vyote vitaniita mimi ni mwenye heri.
49 Kwa kuwa Mwenye nguvu amenitendea mambo makuu;
Na jina lake ni takatifu.
50 Na rehema yake ni kwa vizazi na vizazi,
Kwa wale wamchiao.
51 Ameonyesha uweza kwa mkono wake;
Amewatawanya wenye kiburi katika mawazo ya mioyo yao.
52 Amewashusha wenye viti vya enzi,
Na kuwapandisha walionyenyekea.
53 Amewashibisha wenye njaa kwa vitu vizuri;
Na matajiri amewaaga mikono mitupu.
54 Amemsaidia Israeli mtumishi wake,
Ili aikumbuke rehema yake,
55 Kama alivyosema na baba zetu,
Kwa Ibrahimu na uzao wake hata milele.
#music #gospelverse

